Moshi: Mfanyabiashara Ajimwagia Petroli na Kujipiga Kiberiti hadi Kufa
HILI ni tukio la aina yake ambalo limeacha gumzo na simanzi kubwa baada ya mfanyabiashara wa mjini Moshi, Romani Shirima (74), ambaye ni mmiliki wa Shule ya Sekondari ya Merinyo iliyopo mjini Moshi, kujiua kwa kujilipua kwa petroli nje ya nyumba yake.
Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mfanyabiashara huyo alijifunika kwa blanketi, kisha kujimwagia petroli na kutumia kibiriti kuwasha moto ambao ulimlipua na kusababisha kifo chake.