×

Mashindano ya Suka Suka Ya Times FM Yateka Mwembeyanga

sukasuka-1

…Shughuli mbalimbali kwenye mashindano hayo zikiendelea.

sukasuka-2

Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika Shindano la SukaSuka Mtaa kwa Mtaa linaloratibiwa na Radio Times FM  100.5  katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es salaam.

sukasuka-3

Mmoja wa wananchi  aliyefika viwanjani hapo akiuliza swali namna ya kushiriki shindano hilo.

sukasuka-4

…Shughuli mbalimbali zikiendelea viwanjani hapo

sukasuka-5

Baadhi ya wasusi wakiendelea kusukana katika mashindano hayo.

sukasuka-6

Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye Viwanja hivyo vya Mwembeyanga kushuhudia mashindano hayo.

sukasuka-8

Mtangazaji wa kituo cha Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ anayetangaza kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani akizungumza jambo katika shindano hilo.

sukasuka-9

Mashabiki wakifuatilia mashindano hayo.

VIJANA wametakiwa kuacha tabia ya kuchagua kazi kwa vigezo vya jinsia kwani kazi zote ni muhimu ili mradi ni halali na zinazoweza kukuingizia kipato na kukukwamua kiuchumi.

Hayo yamesemwa Mwembe Yanga jijini Dar es salaam Septemba 30 na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika shindano la SukaSuka Mtaa kwa Mtaa linaloratibiwa na Times FM Radio 100.5

Shindano la sukasuka Mtaa kwa Mtaa lina lengo la kuvumbua, kushindanisha na kupata mshindi katika sanaa ya ususi ambayo inaonekana kusahaulika katika jamii.

Meneja Uhamasishaji wa 100.5 Times FM Namiundu Ngudupale amesema mpaka sasa wamefanikiwa kupata washindi zaidi ya 70 katika shindano hilo ambalo linafanyika mtaa kwa mtaa jijini Dar es Salaam.

Amesema katika kila shindano wanapata washindi watatu ambao wanajinyakulia zawadi mblimbali ikiwemo vifaa vya kwa ajili ya shughuli ya ususi kutoka kwa wadhamini Darling Hair, Coca Cola na Vodacom Tanzania.

Katika shindano hilo ambalo limefanyika katika viwanja vya mwembeyanga temeke jijini Dar es salaam zaidi ya washiriki 15 akiwemo mwanaume mmoja walijiotokeza katika shindano hilo.

Mshindi wa shindano hilo Richard Antony amesema kuwa anawashukuru 100.5 timesfm kwa kuandaa shindano hilo lenye lengo la kuwainua vijana hususani wa hali ya chini.

Baadhi ya wananchi wameipongeza times fm kwa kuvumbua na kuanzisha shindano hilo kwa kuwa litasaidia jamii kuthamini sanaa ya ususi.

Wadau wakubwa wa masuala ya ususi kampuni ya Darling kupitia kwa meneja masoko Rebeka Mbeke amewataka wananchi waendelee kushiriki kwa wingi katika shindano hilo na kwamba wataendelea kutoa zawadi kwa washindi.