×

Amber Lulu Afungukia Kukamatwa Na Unga

amberlulu

Video queen matata Bongo, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’.

Stori: Hamida Hassan, Wikienda

Dar es Salaam: Kufuatia madai ya kukamatwa akisafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ jijini Arusha kuelekea China, video queen matata Bongo, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ amefungukia ishu hiyo akidai kuwa anaamini ilitengenezwa na watu walioamua kumchafua.

14373936_1112266632160075_259230258752913408_n

Amber Lulu akiwa katika pozi.

Amber Lulu aliliambia Wikienda kuwa alishangaa kuona mitandaoni kwamba amekamatwa na unga, lakini hakuna kitu kama hicho kwani hajawahi kukamatwa.

Kabla ya kumpata Amber Lulu, simu yake ilikuwa haipatikani hivyo Wikienda lilimtafuta mdogo wake aliyeko jijini Mbeya ambaye naye alikiri kutompata mrembo huyo hewani kwa siku tatu ambapo ndugu walimtafuta kwenye vituo vya polisi jijini Arusha bila mafanikio.

Wapo baadhi ya watu waliodai kuwa ni kiki iliyofanywa na Amber Lulu mwenyewe ili kuwafanya watu wamuongelee.