The House of Favourite Newspapers

Sekondari Mtakuja, Dar, Haina Walimu wa Hisabati

1-1

Wananchi wa Tegeta-Nyuki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, alipokuwa katika ziara ya kutatua matatizo yanayowakabili.

1-2

Ali Hapi akiongea na wananchi katika ziara yake.

1-3

…Akiongea na wananchi, kushoto kwake ni Diwani Michael Urio.

1-4

Wafanyabiashara wa soko la Tegeta-Nyuki wakionyesha biashara zao kwa Hapi.

1-5

 Hapi akiwa na Diwani Michael Urio (kulia).

SHULE ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi jijini Dar ina uhaba walimu wa hisabati, hali iliyosababisha, diwani wa kata hiyo kutafuta mwalimu ambaye anamlipa mshahara kwa kufundisha somo hilo.

Akizungumza jana katika ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, Diwani wa Kata ya Kunduchi Michael Urio alisema kuwa shule hiyo ina uhitaji wa mwalimu wa somo hilo kwa kidato cha kwanza na pili.

“Nilivyoona kuna uhitaji wa mwalimu wa hisabati kidato cha kwanza na cha pili, niliamua kutafuta mwalimu ambaye ninamlipa mshahara ili aweze kuwasaidia watoto hao,” alisema.

Aidha diwani huyo alisema wanafunzi hao wamekuwa katika mazingira kama hayo tangu mwezi Februari mwaka huu mpaka sasa na wala hakuna dalili za kupatikana mwalimu wa serikali.

Mkuu huyo wa wilaya alimuahidi diwani huyo kuwa atawasiliana na waziri wa TAMISEMI ili waangalie uwezekano wa kupata mwalimu wa somo hilo shuleni hapo.

Hapi alikuwa katika ziara ya kutembelea ziara ya kusikiliza kero za wananchi na kutatua matatizo yanayowakabili.

Na Hilaly Daud/GPL

Comments are closed.