ITALY: Ligi ya Klabu Bingwa Barani Ulaya imeendelea tena usiku wa kuamkia leo ikiwa bado katika hatua za makundi huku mchezo wa kusisimua zaidi ukiwa ni kati ya Legia Warsaw dhidi ya Real Madrid ambao ulikuwa wa piga nikupige.
Katika mchezo huo imeshuhudiwa Gareth Bale aliyeongeza mkataba wa miaka miwili mwanzoni mwa wiki hii na kumfanya alipwe Euro 346,000 kwa wiki, akifungia Klabu yake ya Madrid goli la kusisimua zaidi ambalo ni la mapema zaidi kwenye historia ya UEFA (sekunde ya 58).
Mwanzoni mwa mchezo huo, Madrid walionekana kuwaadhibu mabeki wa Legia Warsaw kwani walikuwa wakilisakama lango la wapinzani wao hao mara kwa mara.
Matokeo ya mwisho Legia Warsaw 3-3 Real Madrid.
Monaco ikiwa nyumbani imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya CSKA ya Moscow.
Tottenham Hotspur pia ikiwa nyumbani katika dimba la Wembley ilikubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Bayer Leverkusen.
Leicester City ikiwa ugenini ililazimishwa sare tasa dhidi ya FC Copenhagen.
Borussia Dortmund 1-0 Sporting
FC Copenhagen 0-0 Leicester city
FC Porto 1-0 Club Brugge
Juventus 1-1 Lyon1
Sevilla 4-0 Dinamo Zagreb
Legia Warsaw: Malarz, Bereszynski, Rzezniczak, Pazdan, Hlousek, Kopczynski, Moulin, Guilherme, Odjidja (Jodlowiec 87), Radovic (Prijovic 77), Nikolic (Kucharczyk 69)
Subs not used: Cierzniak, Jodlowiec, Czerwinski, Hamalainen, Broz
Real Madrid: Navas, Carvajal, Nacho, Varane, Fabio Coentrao (Asensio 77), Bale, Kovacic, Kroos, Ronaldo, Morata (Diaz 85), Benzema (Vazquez 65)
Subs not used: Casilla, Isco, Danilo, Tejero
Referee: Pavel Kralovec

