IKULU, DAR ES SALAAM: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 04 Novemba, 2016 amefanya mahojiano ya kwanza na waandishi wa habari tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita.
Jibu la Rais John Magufuli: Nchi ina umoja, upendo na mshikamano. Kila mmoja ajitahidi kufanya kazi, iwe ya viwanda, makusanyo bil 800 hadi tril 1.2.
Asilimia 40% ya bajeti imeelekezwea kwenye kuboresha miundombinu
Makandarasi zaidi ya 40 wameanza kufanya kazi, reli ya standard gauge kuanzia Dar hadi Morogoro inaanza kujengwa kwa awamu ya kwanza hivi karibuni.
Ndege zote mpya tulizonunua hivi karibuni zimelipiwa cash, hatudaiwi. Bombardier Dash8 Q400, tumefanya order ya ndege nyingine 3, na kuzilipia advance payment, jet mbili (ya kubeba watu 140) na bombardier moja.
Dola milioni 10 zimetengwa kwa ajili ya manunuzi ya ndege ya 4 yenye uwezo wa kubeba watu 240 itakuja 2018 ili kuboresha sekta ya utalii.
Rais Magufuli amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2018 serikali itakua imenunua jumla ya ndege 7 kusarifisha abiria ndani na nje ya nchi.
Fly over ya Tazara, Dar es Salaam.
Serikali imetenga pesa Tsh. Trilioni 1.56 kwa ajili ya kilimo, wawekezaji wamejitokeza Wajerumani kujenga kiwanda Lindi na kitakuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 10,000.
Kuongezeka kwa bei ya mazao mfano korosho kutoka Tsh. 1000 hadi Tsh. 4000.
Nishati: Bajeti yake ni Tril 1.3, mtambo wa Kinyerezi 1 kufanyiwa extension kuongeza uzalishaji wa umeme.
Kinyerezi 2 imeongezwa, Kinyerezi 3 na 4 zinatarajiwa kuanzishwa na kuongeza uzalishaji wa umeme.
Elimu: bajeti ni tril 4.47, elimu bure. Bil 18.77 kila mwezi tukatoa, changamoto wanafunzi wakaongezeka, madawati pia japo inakaribia kuisha.
Mikopo bil 348 zilizotengwa, kuongeza hadi bil 473, wanafunzi 100320, bil 483 kwa ajili ya kukopesha zimetengwa. Wanafunzi hewa, vyuo vikuuu na shuleni.
Maji tril 1.2
Tunaelekea vizuri tuko pazuri. Ya kwanza code va, inflation rate imeshuka.
Uchumi wa nchi yetu mwaka jana ulikua kwa asilimia 7, tumelenga mwaka huu ukue kwa 7.2%. Amesema Rais Magufuli.
Nimealikwa mialiko 47 nimeenda mitatu, nimeacha vikao vingi vya nje, mabalozi watatuwakilisha.
Marais kutoka nje wametuheshimu na kututembela na tumeingia nao mikataba mbalimbali. Tumepanga Tanzania kuwa ya viwanda.
Nimebana matumizi, nimepunguza sherehe ili kuboresha maendeleo nchini.
Kuna madini ya graphite ambayo ndio yanatumika katika magari yanayotumia umeme. Tanzania ni tajiri kinachotakiwa ni namna gani tutatumia hivyo vyanzo.
Tido Muhando: Unawezaje kuzungumzia Baraza la Mawaziri uliloliunda.
Jibu: Mawaziri wanafanya kazi zao vizuri, ni mawaziri wachache lakini wako committed kuwasaidia wananchi na wanafanya kazi zao vizuri kuwatumikia wananchi.
Lulu Sanga TV1: Watoto wadogo wanakufa kwa kukoswa dawa, utenge kiasi kidogo kiende kila hospitali ya wilaya na dispensary kubwa ili kuwasaidia watoto wenye pneumonia.
JMP: Tuneongeza bajeji, tumeagiza madawa moja kwa moja kutoka viwandani kupitia MSD na sio madalali.
Nchi ya Morocco inaanzisha viwanda kwa ajili ya kutengeneza madawa hapa nchini.
Rais Magufuli amesema serikali imezungumza na Morocco ianzishe safari za ndege toka Casablanca hadi Dar es Salaam ili kuongeza pato la utalii nchini.
Sami Awami BBC Swahili: Amemuuliza Rais Magufuli kwamba, watu wengi wanahisi anakandamiza demokrasia ya nchi.
JPM: Sija-supress demokrasia ila nimepromote demokrasia, baada ya uchaguzi lazima watu waendelee na kazi. Mikutano ya ndani ya vyama vya Siasa inaendelea, Bunge linaendelea, wao wenyewe ndio wanaogombana.
Tido: Anauliza swali kwa Rais Magufuli: “Watu wengi wanadhani kwamba unaendesha nchi kidikteta.
JPM: Hiyo ni perception ya watu kila mtu ana mtazamao wake. Katika kazi yoyote, kukosolewa au kupongezwa ni kitu cha kawaida. Sijaibaka demokrasia ya nchini tangu niingie madarakani.
Swali: Mwandishi wa Magazeti ya serikali: Watanzania kuchangamkia fursa zilizopo nchi nyingine.
JPM: Kiswahili, kila mmoja ajipange asitegemee serikali imfanyie kila kitu.
Tanzania ni mwanachama wa SADEC yenye watu zaidi ya milioni 400, watanzania hatuchangamkii fursa, niwaombe Watanzania wachangamkie fursa ili kuboresha maendeleo ndani na nje ya Tanzania ya nchi yetu.
Tido: Jinsi ya ulivyofanikiwa kudhibiti suala la rushwa.
JPM: Swala la rushwa sio la rais peke yake, ni la kila mtanzania, tumeumia kweli kweli, rushwa ni kansa ya maendeleo yetu. Nashukuru nidhamu ya kazi imerudi, wanahabari mna wajibu mkubwa wa kuisaidia nchi yetu. Matunda yameanza kuonekana, tumepitisha sheria ya kupambana na mafisadi, kesi ya kwanza imeanza jana.
Dkt. Ayoub Rioba: Yapi yanakuumiza kichwa?
JPM: Ni mengi ikiwemo ujangiri, madawa ya kulevya, ujambazi na mengine yanaumiza japo tunaenda vizuri. Hata wale wakubwa waliokuwa wanafanya mambo hayo wanashikwa wanapelekwa mahakamani.
Ayoub Rioba kwa Rais Magufuli: Mwaka mmoja umeonesha ujasiri katika masuala mengi ikiwemo ujangili, kitu gani kingine unakipa kipaumbele?
Rais Magufuli anamjibu Ayoub Rioba: “Mwaka mmoja ni mdogo sana lakini tutajitahidi kupambana na hayo yote, dawa za kulevya, ujangili n.k
Mambo ya kulipeleka taifa mbele yanahitaji sapoti ya watu wengi, haya mambo ya ujangili, unga, ujambazi… nafikiri tunaenda vizuri.
Tuma Dandi wa Mlimani FM: Watu wenye ulemavu wana hali mbaya sana, tunashukuru umewateuwa wengine kuwa viongozi kazaa wengi walemavu. Tunaomba uwaangalie walemavu kuhusu biashara, ajira na vitimwendo ikiwemo pia kuondolewa kodi.
JPM: Kila mmoja ni mlemavu wa kesho, nimeunda wizara maalum kwa ajiri ya walemavu, nimeteua mawaziri na viongozi wengine wengi ambao ni walemavu. Sisi wote ni wamoja.
Mhariri Machumu wa Mwananchi: Wafanyabiashara wanahisi kama wametengwa.
JPM: Wafanyabiashara hawajatengwa, bali nataka wafanyabiashara ambao wanalipa kodi. Nataka biashara ambayo iko balanced, wafanyabiashara matapeli siwapendi. Wanawaumiza wafanyabiashara walio wakweli.
Kuhusu madini, madini tuliopewa na Mungu yanatakiwa yainufaishe Tanzania, ndiyo maana tukatengeneza bomba kutoka Hoima kuja Tanga, Tanzania.
Joseph Kulangwa: Kuhusu kusomesha mafundi wa viwandani na Veta
JPM: Tunaendelea kupromote watu waweze kufungua vyuo vya veta na vya mafunzo kama hayo. Vyuo vingi vya ufundi na fani mbalimbali vilibadilishwa kuwa vyuo vikuu. Mfano Chuo cha usafirishaji NIT, Chuo cha Uongozi Mzumbe na vingine.
Swali la Tido Muhando kwa Rais Magufuli: Suala la walimu bado halijaimarika ukizingatia walimu wanafanya kazi ya kipekee, nini unafanya kuhusu walimu.
JPM: Suala la ualimu ni mtambuka lakini mpaka sasa nikuhakikishie, mimi mwenyewe ni mwalimu, elimu imeimarika
Elimu tunaboresha, shule za serikali pia zimekuwa zikiongoza mfano Moa wa Katavi na Geita, madai ya walimu 63,000 yamelipwa na bado madai 39,000.
Madai ya pension tuliingia kulipa bil 187, baadaye tukalipa bil 87. Kwa hiyo tunaendelea kulipa huko tawala za mikoa tumepeleka bil 177. Waliozea pesa za chai sasa hivi hazipo. Niwaombe waandishi muwaeleze Watanzania kuwa tunelekea vizuri. Ndiyo maana nikapeleka 40% kwenye maendeleo ya nchi ambazo kabla ilikuwa ikipelekwa 26% pekee na zingine zilikuwa zikiliwa tu. Sasa hivi hakuna za kutafuna.
Swali: Utamaduni na maadili, kutembea nusu uchi, panya road.
JPM: Kusimamia utamaduni ni suala la kila Mtanzania, kila mmoja wetu ana wajibu wa kusimamia na kusaidia kutoa mwelekeo wa utamaduni wetu. Wanahabari, mna wajibu wa kulinda maadili yetu, unajisikiaje unapomuonesha mtu kwenye TV akiwa nusu uchi au kutoa picha yake front page ya gazeti akiwa uchi na watoto wakaona, hiyo inaporomosha maadili.
JPM: Rais Magufuli amesema mabenki mengi hapa nchini yalikopesha wanasiasa hadi sasa mabenki hayo yameanza kufirisika, wanasiasa wa Chadema na CCM wamo.
Mabenki yanakuja kuikopesha serikali kwa liba ya 60% mwisho wa siku wanaumia wananchi.
Fedha zote zilizopo katika mashirika tunazi-monitor kwa sababu sio zao. Kama ni TANAPA fedha zake zinatokana na utalii.
JPM: Akijibu swali la Tido Muhando, Rais Magufuli amesema kwa sasa hana mpango wa kushughulikia Katiba Mpya, anataka kuinyoosha nchi kwanza kwa kujenga uchumi. Katiba baadaye.
“Sikuwahi kuzungumza suala la katiba mpya wakati wa kampeni zangu, nilitembea km 46000…. tupige kazi kwanza”
Swali la Katibu wamiliki vyombo vya habari (Henry Mhanika): Kumekuwa na mambo ya dharula kupeleka miswada bungeni kuanzia mswada wa takwimu na huu wa huduma ya vyombo vya habari, tunaomba utusaidie.
JPM: Sheria inapopelekwa bungeni inakuwa na makusudi yake kulingana na uhitaji wa wakati ule. Ililetwa 2011, ikawa watu wapewe muda wakajiandae. Kuanzia muda huo mpaka leo watu hawajajiandaa.
Amesema Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ilichelewa kujadiliwa, hatoharibu maamuzi ya bunge, siku ikipitishwa na bunge wakampelekea ataisaini.
JPM: Asema suala la uraia pacha litajadiliwa bungeni.
Kutoka Mwananchi Frank Sanga: Anamhoji Rais Magufuli: Kuna maeneo unapata maksi chache kwenye utawala bora na suala la Zanzibar.
Rais Magufuli kwa Frank Sanga: “Kwenye saikolojia kila mtu anaweza kukupa maksi tofauti, unaweza hesabu ukapata A lakini DS ukapata karai.
“Napenda Constructive Challenges kwa sababu hii nchi ni ya kwetu sote. Hakuna mwenye haki miliki ya nchi”- Rais John Magufuli.
JPM: Hali ya Zanzibar ni shwari, uchaguzi umefanyika na wamempata rais halali ambaye ni Dkt. Shein, sasa mambo yao yanaenda vizuri.
JPM: Tanzanaia ni nchi isiyofungamana na upande wowote, tunashirikiana na nchi zote za Afrika bila kuchagua. Tutashirikiana na nchi yoyote kujenga uchumi wetu.
JPM: Vyombo vyote vya habari navipenda na vinafanya kazi nzuri sana kwenye hii nchi.
Swali la Mayala (Mtangazaji wa Kujitegemea): Mamlaka gani ulitumia kuzuia safari za nje na kuzuia siasa kwa muda.
JPM: Hotuba yangu ya kwanza ya kubana matumizi niliotolea bungeni.
Majaji walilalamika kuwa hawawezi kuamua kesi kwa sababu hawana pesa.
JPM: Nilitoa pesa baada ya muda mfupi, kwa nini hawakwenda kuomba pesa bungeni au kwa Jaji Mkuu? Kwa hiyo lazima tubane matumizi.
JPM: Tulikuwa tunapata hasara kubwa, meli 60 ambazo kila moja inabeba makontena 3000, zilikuwa zinaingia na kutoka hapa nchini na mizigo bila kulipa kodi.
Sikuja hapa kuchimbua makaburi, mengine nitashindwa kuyafukia. Kikubwa mimi nafanya ninayoweza kuyatekeleza.
Nawashangaa wanaolilia kuja Ikulu, nawakaribisha.
JPM: Awaasa wanahabari kuanzisha chama ambacho hata wakitaka kufanya jambo watashirikiana na endapo watamuhitaji atawasaidia.
JPM: Wandishi hata mkisema muanzishe kampuni au kiwanda anzisheni mimi nitawasaidia.
JPM: Nimefarijika sana kuwa na ninyi, hata kama mkiwa na mambo ya kuishauri serikali fanyeni kwenye association yenu mpeni Msigwa ataniletea.
Uchaguzi umekwisha, mimi ndiyo rais wenu, unipende usinipende, uwe wa CCM au wa Chadema mimi ndiyo rais wenu.
JPM: Kuna mambo na mimi natamani kama vile Fiesta ya kesho (Novemba 25) nitakapotimiza rasmi mwaka mmoja madarakani ningehudhuria lakini ndiyo hivyo tena nikitazama jamaa zangu pale (usalama) wamenuna. Siwezi kwenda.
JPM: Rais Magufuli awapongeza wote wasanii na wanamichezo, achukizwa na mashabiki wa Simba na Yanga wanaokwenda kwenye michezo, wakishashindwa wanang’oa viti ambavyo vimetengenezwa kwa gharama kubwa.
Hata hivyo amempongeza Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye kwa hatua alizozichukua kutokana na tukio hilo la mashabiki kung’oa viti, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam wakati wa mechi ya Simba na Yanga, mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Rais Magufuli amemaliza kwa kuwapongeza wnahabari wote kwa kuitikia wito wa kwenda Ikulu kuzungumza naye, pia amewataka wawe wamoja na wajitume kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.
