Mgombea wa Republican, Trump ameshinda urai wa Marekani ambapo mpaka sasa naongoza kwa kura 288, Clinton kura 218 za wajumbe kati ya kura 538.
Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Mshindi alitakiwa kushinda angalau majimbo 270 lakin Bw. Trump amevuka lengo na kufikisha kura 288 mpaka sasa.
Mgombea wa Republican, Trump anaongoza kwa kura 276, Clinton kura 218 za wajumbe, hivyo trump atatangazwa mshindi muda wowote.
Mgombea wa Republican Donald Trump ameshinda jimbo la Pennsylvania kwa asilimia 49 dhidi ya 48 za Clinton. Jimbo hilo lina kura 20 za wajumbe. Clinton sasa ana jumla ya kura 245 za wajumbe na Trump 218. Bwana Trump anahitaji kura 26 tu ili aweze kufikisha kura 270 ambazo atahesabiwa kuwa mshindi.
Clinton kushinda Virginia
ABC News wamekadiria kwamba Hillary Clinton ndiye mshindi jimbo la Virginia, moja ya majimbo yaliyokuwa yanashindaniwa. Jimbo hilo lina kura 13 za wajumbe.
Trump ndiye mshindi Ohio
ABC News wamekadiria kwamba Donald Trump atashinda jimbo muhimu la Ohio. Jimbo hilo lina kura 18 za wajumbe.
Trump ashinda jimbo la Montana
Mgombea wa Republican Donald Trump ameshinda jimbo la Montana. Jimbo hilo lina kura 3 za wajumbe. Clinton sasa ana jumla ya kura 104 za wajumbe na Trump 140.
Trump ‘ana nafasi nzuri’ – New York Times
Gazeti la New York Times, ambalo limekuwa likiunga mkono Hillary Clinton, linasema mfumo wake wa kompyuta kwa sasa unabashiri uwezekano wa Trump kushinda kuwa 53%.
Louisiana kwenda kwa Trump
ABC News wanakadiria kwamba Donald Trump atashinda jimbo la Louisiana.
Jimbo hilo limepigia kura mgombea wa Republican katika chaguzi nne mtawalia lakini waliunga mkono Bill Clinton mwaka 1992 na 1996.
Jimbo hilo huwa halichukuliwi kama ngome ya Republican kama yalivyo majimbo mengine jirani.Jimbo hilo lina kura nane za wajumbe.
Clinton ashinda jimbo la Washington
Hillary Clinton ameshinda jimbo la Washington kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Jimbo hilo lina kura 12 za wajumbe. Sasa Trump ana kura 222 za wajumbe na Clinton 209 za wajumbe. Mshindi anahitaji kura 270.
Trump ndiye mshindi Florida
ABC News wametangaza kwamba makadirio yao yanaonyesha Trump ameshinda jimbo muhimu la Florida.Sasa Trump ana kura 222 za wajumbe na Clinton 197 za wajumbe. Mshindi anahitaji kura 270.
Jimbo hilo huwa muhimu sana kwa mgombea yeyote.
Jimbo hilo lilimpigia Obama mwaka 2008 na 2012 (Democratic), lakini George W Bush (Republican) alishinda uchaguzi uliotangulia 2000 na 2004. Jambo la kushangaza ni kuwa alikuwa mbele na kura 537 pekee mwaka 2000.
Hata hivyo, ilichukua siku 36 kwake kuthibitishwa kuwa mshindi, kwa hivyo iwapo wagombea watakaribiana sana usitarajie matokeo yatangazwe haraka.
Clinton mshindi Connecticut, kwa mujibu wa ABC
Hillary Clinton ameshinda jimbo la Connecticut, ngome ya chama cha Democratic ambapo amejishindia kura saba za wajumbe, kwa mujibu wa ABC News. Clinton sasa ana kura za wajumbe 104 na Trump 129.
Trump mshindi jimbo la Arkansas
Trump anakadiriwa kushinda jimbo la Arkansas kwa mujibu wa ABC News. Jimbo hilo lina kura sita za wajumbe.
Kwa kura za wajumbe, sasa Trump ana 129 na Clinton 97



