×

Mwili wa Mungai Waagwa Dar

msibani-3Mwili wa Marehemu Joseph Mungai ukiwasili Viwanja vya Karimjee, jijini Dar kwa ajili ya kuagwa.msibani-1

msibani-2

msibani-4

msibani-5

msibani-6

msibani-7

msibani-8

msibani-9

DAR ES SALAAM: Mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu, Joseph James Mungai unaagwa hivi sasa katika Viwanja vya Karimjee,  Dar es Salaam.

Viongozi mbalimbali wa kitaifa pamoja na wananchi wamehudhuria katika tukio hilo la kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kabla ya kuusafirishwa kwenda Mafinga, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa kwa ajili ya mazishi.

 Viongozi walifika mpaka sasa ni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt.  Gharib Bilal,  Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Fredrick Sumaye na wengine.

PICHA NA DENIS MTIMA/GPL