
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Mungai.

Marehemu Joseph Mungai enzi za uhai wake.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa akimpa pole mke wa Marehemu Mungai, Mary Mungai.

Makamu wa Rais Mstaafu, Dk. Ghalib Bilal akitoa heshima zake za mwisho.

Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye akiaga mwili wa Mungai.

Jaji Warioba naye akitoa heshima zake kwa mwili wa marehemu.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akisaidiana na waombolezaji kubeba jeneza lenye mwili wa Mungai.

Jeneza lenye mwili wa Mungai likiwa mbele ya waombolezaji.
Mama Salma Kikwete akimfariji mke wa Marehemu Mungai, Mary Mungai.

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akimpa pole mke wa marehemu.
Mzee Kingunge (kushoto) akisalimiana na Phillip Mangula.
Mkapa na Sumaye wakiwa msibani hapo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akitoa neno.
RAIS wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo amemlilia aliyewahi kuwa waziri katika awamu zote nne za uongozi nchini, Marehemu Joseph Mungai ambaye mwili wake umeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli akiwaongoza Watanzania katika kuuaga mwili wa Mungai, alishindwa kuficha hisia zake wakati wa kuaga mwili wa marehemu na kutokwa na machozi, jambo lililopelekea kutoa kitambaa cha mkononi na kujifuta.
Mbali na rais, wengine walioshindwa kujizuia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Lawrence Masha na viongozi wengine.
Viongozi wengine waliofika kuuaga mwili wa Mungai ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu, Dk. Ghalib Bilal, Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Daniel Lubuva, Jaji Joseph Warioba, Mzee Kingunge, Mzee John Cheyo, Steven Wassira, Spika wa Bunge Mstaafu, Pius Msekwa na wengine.
Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho kuelekea Mafinga, mkoani Iringa kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumamosi.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE!
Picha / Habari: Denis Mtima, Gabriel Ng’osha/GPL






