DAR ES SALAAM: HATIMAYE mkali wa wimbo Jike Shupa, Nuh Mziwanda ameamua kuuaga ukapera baada ya kufunga ndoa kimyakimya na mpenzi wake wa muda mrefu aitwae Nawal.
Nawal ndiye alichukua nafasi ya mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa Nuh baada ya wawili hao kutengana huku juhudi za kuwapatanisha zikigonga mwamba.
Ndoa ya Nuh na Nawal imewashtua wengi kwa kuwa hakukuwa na taarifa ambazo pengine watu walitegemea zingesambaa mitandaoni kuhusu lini angefunga ndoa hiyo kama ambavyo hufanya wasanii wengine, lakini cha ajabu watu wamekutana na picha mitandaoni zikionesha tayari Nuh amekwishafunga ndoa na Nawal.
Inasemekana kwa sasa Nuh na Nawal wanajiandaa kufanya bonge la party kusherehekea ndoa yao mpya.
Mastaa wengine waliofunga ndoa hivi karibuni ni pamoja na Masanja Mkandamizaji, Nyandu Tozzy, Tunda Man, Mabeste pamoja na wengine wengi.