×

Nabii wa Nigeria Asema Trump ni Mpinga Kristo Aliyetumwa na Shetani

omaleABUJA: NABII kijana Emmanuel Omale wa Nigeria ambaye alitabiri kwa usahihi matokeo ya uchaguzi wa urais wa Marekani mnamo Mei mwaka huu, amefichua kile alichosema kuwa ni maono aliyopewa na Mwenyezi Mungu kwa wafuasi wa kanisa lake, kuhusu rais ajaye wa nchi hiyo.

Omale amemwelezea Donald Trump kuwa ni mpinga Kristo, ambaye atawalazimisha watu wote duniani kutumia nembo ya mnyama inayoaminika kuwa ni ya Kishetani (Freemasonry) ya 666.

trumppTrump

Nabii huyo ambaye ni mwanzilishi wa Kanisa la Pentekoste jijini Abuja alisema Mungu alimwonyesha kwamba Donald Trump ametumwa na Shetani ili kuleta machafuko, maafa na vita duniani.

omaleeKatika video ambayo aliiweka mtandaoni kwa mara ya kwanza Mei 7, 2016, Omale aliwataka wafuasi wake kumwomba Mungu ili kuepusha vita na umwagaji wa damu ambao utasababishwa na Donald Trump akiingia madarakani baada ya ushindi alioupata juzi.

Juzi, Novemba 9, Trump alishinda urais wa Marekani baada ya kumzidi kura mpinzani wake wa Democratic Bi. Hillary Clinton na ataapishwa rasmi kuwa Rais wa Marekani Januari 20, 2017.

 Baadhi ya maneno ya nabii huyo.omalees

Source: Nigerian Prophet Emmanuel Omale Calls Donald Trump The Antichrist Sent By The Devil

TAZAMA VIDEO