×

Tuzo ya EATV zaivaa

eatv-1Jopo la wadhamani na waandaaji wa tuzo hiyo wakiwa kwa pamoja.

eatv-2Katibu mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania Godfrey Mungereza akizungumza jambo.

eatv-3Muakilishi kutoka kampuni ya Coca Cola ambaye ni mmoja wa dhamini Anna Lugenge akizungumza jambo.

eatv-4  Mmoja waandaji wa tuzo hizo kutoka EATV,Loy akimkabidhi mmoja wa wawaklisha kutoka Vodacom Ibrahim Kaude karatasi ya majina ya wasanii walioingia kwenye kinyanganyiro hicho. eatv-6Tuzo zinazowania kupitia televisheni  ya East Afrika zimeanza kunukia baada ya washiriki wengine walioingia katika kinyan’ganyiro hicho  zenye  vipengele kumi zimetajwa ambapo nia na madhumuni ni kuwatunza  wasanii wa filamu na muziki ambao wamejipendekeza wenyewe kwa kujaza fomu maalum.

 Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari  uliofanyika katika Hoteli ya Sleep Way iliyopo Masaki jijini Dar, mratibu wa shidano hili Roy, alisema kuwa  tuzo hizo zinatarajia kufanyika  tarehe 10 Desemba,katika ukumbi wa Mlimani  City  ambapo wasanii tisa na tunzo moja ya heshima zitatolewa.