Hiroshi Mikitan (kulia) ambaye ni Mmliki wa Kampuni ya Rakuten akiwa na Rais wa Barcelona baada ya kusaini mkataba mpya.
HISPANIA: Klabu ya Barcelona imesaini mkataba mpya na mdhamini aitwaye Rakuten kutoka nchini Japan.
Rakuten ni kampuni ya kuuza bidhaa kupitia mtandaoni na imekubali kumwaga vuba la pauni million 200 kwa mkataba wa miaka minne.
Kuanzia msimu ujao, jezi za Barcelona zitakuwa na nembo ya Rakuten kifuani na kuiacha lie ya Qatar Airways ambalo ni shirika kubwa zaidi.
Imeelezwa kuwa, beki Gerard Pique ndiye aliyezungumza na mmliki wa Rakuten hadi mwisho wakafikia dili hilo.
