Afande Sele Afunga Ndoa na Wema Makongoro Morogoro

Mkali wa Rhymes Tanzania, Rappa Seleman Msindi maarufu kama Afande Sele, amefunga ndoa na mpenzi wake Wema Raphael Makongoro katika sherehe ya kifamilia na kiserikali iliyofanyika mkoani Morogoro.
Sherehe hiyo iliendeshwa kwa mujibu wa sheria za ndoa ya kiserikali, ikihudhuriwa na ndugu, wasanii, jamaa, na marafiki wa karibu. Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Hilary Sagara, ndiye aliyesimamia zoezi la kufunga ndoa.
Kwa Afande Sele, hii ni ndoa yake ya pili, baada ya kufiwa na mke wake wa kwanza, Mama Tunda, ambaye alifariki dunia tarehe 14 Agosti, 2014.
Mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wamesheherekea pamoja naye mtandaoni, wakimtakia heri na maisha mema pamoja na mke wake mpya.

