The House of Favourite Newspapers

Alikiba AMjibu DIAMOND Kimagumashi

 KUFUATIA jana Novemba 5, Staa wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wasafi Media kutangaza kuwa anatamani sana kumuona msanii mwenzake Alikiba akiungana naye kwenye Tamasha lake la Wasafi Festival, Kiba amemjibu Diamond kimagumashi kwa kupost picha ya mchekeshaji maarufu duniani, Mr. Bean na kuandika maneno kadhaa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kiba amepost picha hiyo yenye maneno; ‘Thank you for listening, To my presentation’, halafu chini ya post hiyo akaandika “Your welcome”
Mashabiki wengi wamechukulia kwamba hilo ndio jibu la Alikiba ambalo wamedai ni magumashi, dharau au kejeli ya Kiba kwa Diamond kuhusu suala la yeye kushiriki Wasafi Festival ambayo itaanza November 24, 2018 mkoani Mtwara kisha kwenda Iringa na Morogoro.
Jana, baada ya Diamond kuongea hayo watu walianza kuzungumza mitandaoni na kusema siyo rahisi kwa Alikiba kukubali kuungana na Diamond kwenye Wasafi Festival huku wengine wakisema Alikiba akubali tu, na hadi kufikia wengine kusema Alikiba atatoa jibu lake baya au la kizarau sana.

Comments are closed.