The House of Favourite Newspapers

Aliyemsifia Mama Yake Kuliko Mkewe Afunguka

0

Kutoka mitandaoni kuna ‘video clip’ ili-trend ikimuonesha Michael Jackson akimsifia mama yake mzazi kwenye harusi kuliko mkewe ambapo baadhi ya watu wamejaji tukio hilo kwa kusema sifa hizo alizotoa ilibidi ziende kwa mke wake.

 

Michael Jackson amesema; “Jamii inaishi kwa mitazamo waitakayo, mazoea na kukariri baadhi ya vitu, ukitaka kuwaridhisha hutoweza na utakua mtumwa katika kuishi maisha yako na kile unachokiamini, nafasi ya wazazi inabaki kwenye nafasi yao na mke ana nafasi yake.

 

“Kumsifia mke hakuondoi upendo,shukran na thamani ya wazazi na kuwasifia wazazi hakuondoi thamani na upendo kwa mke, lazima watu waelewe hakuna muda maalumu au siku maalumu anayostahili kupongezwa mzazi, mke au mume, sema mazuri ya mtu popote unapopata nafasi akiwa anasikia kwani hakuna aijue kesho,” ameongeza.

 

Pia ameendelea kusema yeye na mke wake wanajuana vizuri na hawaishi kwa matarajio ya watu bali wanaishi kwa uhalisia ya maisha yao.

Leave A Reply