Amber Lulu: Niacheni Nizae, Kumtaja Baba wa Mtoto

Lulu Euggen ‘Amber Lulu’.

MWANAMUZIKI wa kike machachari kwenye Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ amesema kuwa alichokisema kuwa ni mjamzito ndicho chenyewe kwani yeye ni mwanamke na anastahili kuzaa sasa.

 

Amber Lulu aliliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, kubeba mimba kwake siyo jambo geni kwa mwanamke na ‘soon’ atamuweka wazi baba wa mtoto.

 

“Kubwa ni kumshukuru Mungu kunijalia kupata ujauzito, sioni aibu yoyote kwani mimi ni mwanamke hivyo watu waniache nizae jamani maana umri nao unasonga mbele,” alisema Amber Lulu.

STORI NA IMELDA MTEMA


Loading...

Toa comment