AMBER RUTTY AIBUKA KIVINGINE

MSANII chipukizi wa Bongo Fleva, Rutyfiya Abubakary ‘Amber Rutty’ amevunja ukimya wa muonekano wake baada ya kuibuka kivingine. Kwa mujibu wa chanzo, Amber ameamua kubadilika katika mfumo wa maisha yake ikiwa ni baada ya kutimiza miezi sita tangu afunge ndoa na bwana wake, Said Mtopali.

“Wengi walizoea kumuona Amber yule mwenye kujichetua sana mbele ya kamera, wengine walizoea kumuona muonekano wake wa nywele ukiwa wa rangi kama nyeupe kwa mbali kama anavyojiwekaga Amber Rose wa Marekani lakini sasa hivi ameamua kubadilika. Anavaa mawigi na hata kimavazi yupo tofauti kabisa,” kilisema chanzo.

Katika kuonesha hilo, hivi karibuni Amber aliingia katika studio na kupiga picha akiwa katika mavazi ya Kihindi huku gumzo likiwa ni mwonekano wake ambapo kwanza anaonekana mnene na pia nguo za heshima alizokuwa amezivaa.

Risasi Jumamosi lilimtafuta Amber baada ya kunasa mwonekano wake ambao kwa namna moja unaweza kusema amekuja kivingine ambapo alisema amekuwa akipata mapenzi mazito sana kutoka kwa mumewe kitu ambacho huko nyuma kabla ya kukuta naye hakuwahi kabisa kuona ndiyo maana amebadilika.

“Jamani naweza kusema kuja kivingine hivi ni Mungu tu, amenipa zawadi ya maisha yangu (Said) ananipenda sana na mimi nampenda amenifanya nimeonekana mwanamke katika wanawake wengine hivyo ndani ya miezi sita hii nilioishi naye namuomba Mungu aniongezee miaka mingi mingine mbele ili niweze kuwa naye siku zote,” alisema Amber Rutty. Amber Rutty amejizolea umaarufu baada ya video yake kuvuja inayoonesha akifanya ngono kinyume na maumbile.

Loading...

Toa comment