The House of Favourite Newspapers

Amunike Aishitaki TFF FIFA Akitaka Pesa Zake Haraka

Kocha aliyeipeleka Tanzania kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019, Emmanuel Amuneke amelishtaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) akilalamika kutolipwa stahiki zake.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Kocha huyo ambaye ni raia wa Nigeria ameamua kupeleka shauri hilo FIFA ili waweze kulitatua.

 

TFF walifikia uamuzi wa kuvunja mkataba na Amuneke baada ya Taifa Stars kufanya vibaya katika fainali za AFCON zilizofanyika kati ya Juni 21 hadi Julai 19.

Comments are closed.