AS Roma waweka Rekodi Kwenye Kiswahil
KLABU ya AS Roma ya Italia imeweka rekodi ya dunia kwa kuwa klabu ya kwanza kufungua akaunti Twitter, inayotumia lugha ya Kiswahili kutoka Ulaya.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya mashabiki wa timu hiyo waishio nchi za Kenya, Uganda na Tanzania kuomba uongozi wa klabu hiyo kufungua akaunti ya Twitter itakayokuwa inatoa taarifa kwa Lugha ya Kiswahili.
Rais wa AS Roma, Jim Pallota alithibitisha jambo hilo kupitia ukurasa wao wa Twitter kwa kuandika kwa lugha ya Kiswahili: “Kama mnahitaji ukurasa wa AS Roma wa Kiswahili kweli mnastahili kuwa nao, amani na upendo kwenu nyote.” Akaunti hiyo mpya imezinduliwa siku nne zilizopita na inatambulika kwa jina la AS Roma Swahili.
Kuzinduliwa kwa akaunti hiyo kunamaanisha AS Roma sasa itakuwa inatoa taarifa za klabu hiyo katika lugha 14 tofauti kwenye mitandao ya kijamii, Kiswahili, Kiitaliano, Kiingereza, Kiarabu, Kiindonesia, Kihispania, Kifaransa, Kireno, Kibosnia, Kituruki, KiUholanzi, Farsi, Pidgin na Kichina
Comments are closed.