The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kuirejesha Azam Kimataifa, Chirwa ajisogeza Yanga

STRAIKA anayepambana kwa udi na uvumba arudishwe Yanga, Obrey Chirwa juzi Jumamosi aliipa Azam tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Chirwa amewaambia marafiki zake kwamba ana hamu sana ya kurudi Yanga lakini Spoti Xtra linajua kwamba Mwinyi Zahera amewaambia viongozi ; “Achaneni nae…mkaushieni.”

 

Azam waliifunga Lipuli FC bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya FA uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi na kuhudhuriwa na utitiri wa mashabiki ambao mpaka wengine walikosa sehemu ya kukaa.

Chirwa aliibuka shujaa wa mchezo huo akifunga bao kwa shuti kali baada ya kumzidi ubavu beki kisiki wa Lipuli FC, Paul Ngalema na kutumbukiza mpira kambani dakika ya 64.

 

Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, wengine ni Raisi wa shirikisho la soka Tanzania TFF Walace Karia ambaye aliambatana na mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi.

Nahodha wa Azam Agrey Moris ambaye aliibuka mchezaji bora wa mashindano hayo na kusema; “imekua furaha kubwa sana kwangu na kwa wachezaji wenzangu baada ya kufanikiwa kutwaa kombe na kuipeleka timu katika michezo ya kimataifa.”

 

Wengine waliotwaa tuzo ni pamoja na Paul Ngalema akiibuka mchezaji bora wa mechi na Seif Rashidi wa Lipuli akiwa mfungaji bora akitupia kambani mabao manne.

Comments are closed.