
MSANII wa Bongo Fleva, kutoka Label ya WCB Wasafi, Mbwana Yusuph Kilungi maarufu kama Mbosso Khan amefunguka kufanya maajabu ya burudani kwa mashabiki wake usiku ya Christmasi, Desemba 25, 2019 katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live

Kupitia kipindi cha Bongo255 kinachorushwa na +255 Global Radio, Mbosso amesema kuwa, amejipanga vilivyo kuwadhihirishia mashabiki zake kuwa yeye ni msanii bora na hayupo kwenye game kimakosa.

“Nimejipanga vilivyo kukiwasha pale Dar Live, Christmas hii, nimejiaandaa vya kutosha, nita-perform na Live Band, pia nitakuwa nafanya Playback, kwa hiyo utaona sio kazi ya kitoto, watu waje kwa wingi kuona balaa nitakalolifanya pale Mbagala,” alisema Mbosso

Aidha, msanii huyo alisema katika usiku huo uliopewa jina la “Tamu za Mbosso” hatakuwa peke yake bali ataambatana na wasanii wengine wa Bongo Fleva kutoa Burudani Mbagala ambapo ndipo mahali alipokulia kisanaa msanii huyo.

“Nitakuwa na Young Killer, Chid Benz, Zee Cute, Enock Bella na wengine wengi ambao tumjipanga kutoa burudani ya kufa mtu,” alimalizia Mbosso.
View this post on Instagram
View this post on Instagram