Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo na Acting Colonel Joseph Bakari wakisikiliza maelezo kabla ya hatua ya kumvua cheo cha zamani na kumvika kipya
Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akimvisha cheo kipya Colonel Joseph Bakari.
Hafla hiyo fupi iliyohudhuriwa na ujumbe wa Watanzania waliohudhuria Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Jijini Berlin Ujerumani akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma, Mshauri wa Rais wa Zanzibar mambo ya Utalii na Utamaduni Mhe. Chimberi Heri, Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Mhe.
Akitoa maelezo mafupi kuhusu tukio hilo Mhe.
Akisoma sehemu ya maelekezo hayo alisema “ kwa kawaida Afisa anapopanda cheo akiwa nje ya nchi iwapo hataweza kwenda Tanzania kuvalishwa cheo hicho na viongozi husika wa JWTZ, cheo hicho kipya huvishwa na Afisa Mkuu au Balozi wa Tanzania katika Nchi aliyepo”.
Hivyo, kwa mujibu wa sheria na mamlaka aliyekuwa nayo anatakiwa kumvisha Cheo kipya cha ukanali mhusika kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Akitoa nasaha fupi na salam za pongezi kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, wageni waliohudhuria hafla hiyo na Watanzania wote kwa ujumla kwa Kanali Bakari aliyefuatana na Mkewe Bi Lucy Mlingi, Mhe. Balozi alimkumbusha Kanali Bakari kuwa ni dhahiri kuwa kupandishwa kwake cheo kumetokana na imani ya Mkuu wa Majeshi na viongozi wengine wakuu katika utendaji wake,uadilifu, bidii katika kazi na utii.
Comments are closed.