Barcelona Yafuta Uteja Wa Miaka 9 Kwa Bayern Munich
Mei 7 2015, ilikuwa mara ya mwisho Kwa Klabu ya Barcelona kuifunga Bayern Munich ‘The Bavarians’ mabao mawili ya Lionel Messi pamoja na Neymar Junior yalitosha kuwaangamiza Bayern, imepita miaka 9 na miezi mtano tangu siku hiyo timu hizo zikikutana mara sita kabla ya mchezo wa Jana na michezo yote Bayern Munich wamewabuluza wakatalunya hao bila huruma, na hapo Jana amefanikiwa kufuta uteja huo.
Barcelona amekumbana na vipigo vya aibu katika kipindi hicho, huku kumbukumbu mbovu zaidi ni pale alipopokea kipigo Cha aibu Cha mabao 2-8 katika msimu wa 2019/2020, wakati Mshindi wa Ballon D’or mara nane Lionel Andress Messi akiwa mmoja wa waongoza jahazi lilolazamishwa bila huruma.
Kabla ya mchezo wa Jana, ambao ulikuwa ni mchezo wa Saba tangu mei 7, 2015. Historia inaonyesha Bayern ameshinda jumla ya magoli 22-4 katika michezo sita ambapo alishinda 3-2, 2-8, 0-3, 3-0, 2-0, 3-0 kabla ya uteja kumalizika na Barcelona kushinda bao 4-1 pale kwenye dimba la Lluis Olimpic.
Historia zinawabeba zaidi Bayern Munich wanapokutana na Barcelona kwani timu hizo zimekutana mara 14 , Bayern akishinda mara 10, Barcelona mara 3 na wakitokea sare mara Moja tu katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya, lakini hiyo ni tofauti Kwa Los blancos kwani Kwa kipindi kirefu mahasimu wa Barcelona Real Madrid wamekuwa wakibuka washindi mbele ya Real Madrid.
Shukrani ziwaendee Raphina na Robert Lewandowski wakiwa pamoja na vijana wadogo kutoka La masia waliofanikisha shughuli hiyo, chini ya kocha wa zamani wa Bayern Munich Hans Flick Kwa pamoja wameshirikiana kuvunja uteja huo uliodumu Kwa kipindi Cha miaka tisa.