Beki wa Arsenal Gabriel Apambana na Majambazi Gereji Kwake

Nyota wa Klabu ya Arsenal, Gabriel Magalhaes amekabiliana na wezi waliokuwa wameficha nyuso zao na kujihami kwa silaha ikiwemo marungu ambao walivamia katika gereji ya mwanasoka huyo na kujaribu kuiba gari lake.

 

Wezi hao ambao walikuwa watatu walimfuata Gabriel kimya kimya mpaka nyumbani kwake eneo la Barnet London Agosti 20, mwaka huu na kumtaka awapatie funguo zake za gari lake.

 

Kanda ya video ya tukio hilo ambayo imeonekana juzi inamuonesha Gabriel akijaribu kukabiliana na mtu aliyebeba rungu la mchezo wa baseball ambaye baadaye alijulikana kama Abdi Muse.

 

Muse mwenye umri wa miaka 26 alihukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa makosa ya wizi wa kutumia nguvu katika mahakama ya Harrow Crown mnamo tarehe 17 Novemba.

 

Baada ya kuzidiwa nguvu mwizi huyo alitoroka na funguo za gari la Gabriel lakini akaliwacha gari hilo nyuma katika gereji. Baadaye jamaa huyo alikamatwa na maafisa wa polisi na kushtakiwa na wizi wa mabavu na kumiliki silaha hatari.705
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment