The House of Favourite Newspapers

Watu zaidi ya 78 Wafariki Baada ya Boti Kuzama Ziwa Kivu, Mashariki mwa Congo

Watu zaidi ya 78 kufikia leo Oktoka 4, 2024 wamefariki dunia huku wengine wengi wakiwa hawafahamiki walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Kivu, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ajali hiyo imetokea Alhamisi, Oktoba 3, 2024 ambapo chanzo kinatajwa kuwa ni boti hiyo kuelemewa na mizigo pamoja na abiria waliokuwa wengi kuliko uwezo wake.

Kulikuwa na abiria 278 ndani ya boti hiyo, kulingana na gavana wa mkoa, Jean Jacques Purisi.

Picha zilisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii jana, zikionesha vikosi vya uokoaji vikijaribu kuokoa maisha ya watu wengi walioopolewa kwenye mto huo, huku video nyingine ikidaiwa kuwa ndivo jinsi boti hiyo ilivyozama.

Mwanaharakati wa eneo hilo, Aaron Ashuza, ambaye alikuwa katika eneo la tukio, amesema kwamba aliona miili ikitolewa nje ya mto na kwamba majeruhi wamepelekwa hospitalini.

BLACK PASS KIZIWI: RAFIKI YAKE APATA UKIMWI KWA MUME wa MTU BAADA ya KUACHANA na BOYFRIEND MASKINI!