The House of Favourite Newspapers

BRANDY; MTOTO WA NYOSHI EL SAADAT ALIEVAMIA ‘GAME’

Brandy Nyoshi el Sadaat

UPO msemo kuwa mtoto wa nyoka ni nyoka! Yaani anachofanya baba au mama basi na mtoto naye anaweza kufuata nyayo hizohizo.  Ukiachana na huo usemi, kwenye muziki tumekuwa tukiona wasanii wengi wakifuata nyayo za wazazi wao, mfano Komandoo Hamza Kalala ambaye mwanaye, Kalala Junior anakimbiza katika Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, yupo Zahir Ally Zorro ambaye mwanaye Banana Zorro anatamba na Bendi ya B Band, yupo mtoto wa marehemu TX Moshi, Hassan TX au TX Junior anayetamba na bendi ya Msondo Ngoma.

Lakini kwenye Muziki wa Bongo Fleva kuna igizo jipya kwa upande wa wanamuziki wa kike ambaye ni Brandy Nyoshi el Sadaat mtoto wa mkongwe wa Muziki wa Dansi, Nyoshi el Sadaat. Jina la Nyoshi lilikuwa kubwa zaidi alipokuwa akiitumikia Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ kabla ya kumiliki bendi yake mwenyewe ya Bogos. Tangu amekuwa katika bendi hizo hajawahi kuonekana hadharani na binti yake huyo.

Mikito Nusunusu limefanikiwa kumchimbua Brandy na kufanya naye Exclusive Interview na katika makala haya anafunguka zaidi muziki na maisha yake kwa ujumla…

MIKITO NUSUNUSU: Unaweza kutuambia umezaliwa wapi, Bongo au Kongo?

BRANDY: Nimezaliwa hapahapa Tanzania

MIKITO NUSUNUSU: Mama yako ana asili ya Kongo kama baba?

BRANDY: Hapana, mama yangu naye ni Mtanzania tu.

MIKITO NUSUNUSU: Una umri gani?

BRANDY: Kwa sasa nina miaka ishirini.

MIKITO NUSUNUSU: Wewe ni mtoto wa ngapi kuzaliwa?

BRANDY: Ni mtoto wa pili.

MIKITO NUSUNUSU: Baba yako ni Mkongo, je, umeshawahi kwenda Kongo japo kuishi kwa siku chache?

BRANDY:Yeah nimewahi kwenda mara nyingi tu.

MIKITO NUSUNUSU: Mara ya mwisho kwenda Kongo ni lini?

BRANDY: Ni mwaka jana.

MIKITO NUSUNUSU: Ulipofika Kongo ulipokelewaje na ndugu zako maana wewe umezaliwa Tanzania?

BRANDY: Nilipokelewa vizuri na wananipenda sana.

MIKITO NUSUNUSU: Ni kitu gani kilichokuvutia mpaka ukaamua kuimba Muziki wa Bongo Fleva na isiwe Muziki wa Dansi kama baba yako?

BRANDY: Ni mapenzi tu ya Muziki wa Bongo Fleva, pia sijapenda niimbe muziki unaofanana na wa baba yangu.

MIKITO NUSUNUSU: Baba yako amekuwa akijisifu sana kwamba anafurahi kukupata wewe mtoto ambaye unafuata nyayo zake kwenye muziki, je, yeye huwa anahusika kukufundisha?

BRANDY: Kipaji ninacho naweza na sijafanya muziki kwa sababu baba yangu anaimba, mimi kipaji changu ni kuimba na ninapenda muziki.

MIKITO NUSUNUSU: Ulishawahi kufanya nyimbo yoyote na baba yako?

Brandy: Hapana, bado sijafanya.

MIKITO NUSUNUSU: Umeimba nyimbo ngapi na je, umesharekodi?

BRANDY: Nyimbo nyingi tu tayari na zote nimerekodi Studio ya AM Records chini ya Bob Manecky.

MIKITO NUSUNUSU: Una mpango gani na huo muziki wako kwa sasa na baadaye?

BRANDY: Nahitaji nifike mbali kama wengine walipofika na mimi nije kusaidia familia yangu, nifanye juhudi nisimwangushe baba yangu.

MIKITO NUSUNUSU: Changamoto gani unazokutana nazo kwenye muziki?

BRANDY: Nakutana na changamoto nyingi kwa sababu mimi ni msichana mzuri na napendwa na wengi, kwa hiyo leo unapotaka kufanya kitu fulani au una hamu nacho kukifanya lazima uhangaikie na kuhangaikia lazima utafute watu muhimu wa kuweza kufanya jambo lako liendelee, ndiyo utakutana na mtu anayekutaka kimapenzi mfano prodyuza au wanamuziki wengine ili aweze kukusaidia lakini unatakiwa kujitambua na kujua nini unafanya, kikubwa ni kusimamia kazi yako.

MIKITO NUSUNUSU: Unajisikiaje baba anavyokusapoti?

BRANDY: Najisikia vizuri na najivunia kupendwa na baba yangu, nalijua hilo kama napendwa sana.

MIKITO NUSUNUSU: Tunaona watu wa Kongo wanapenda sana kutumia vipodozi hasa wanaume na baba yako, Nyoshi pia ni mmoja wa watumiaji wa vipodozi hivyo, kwako unalichukuliaje hili?

BRANDY: Ujue kila mtu anataka ang’ae kwenye kamera hata mwanamke utakuta lazima apakae make up ndo’ aende sehemu aonekane, mimi sioni cha ajabu, sishtuki, sichukii, kila mtu na life style yake.

MIKITO NUSUNUSU: Upo katika uhusiano?

BRANDY: No comment.

Mikito Nusunusu: Una nyimbo gani kwa sasa?

BRANDY: Sijaanza rasmi kuzitoa, namalizia kurekodi na mtazisikia soon muda ukifika, muziki

Comments are closed.