The House of Favourite Newspapers

BREAKING: KOCHA WA SIMBA APEWA MKATABA WA MWAKA MOJA

Pichani ni Kocha Aussems (kushoto) akisaini mkataba, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Simba, Swedi Mkwabi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo, Mohammed Dewji. 

Kocha wa Simba Patrick Aussems amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuinoa timu hiyo.

Hatua hiyo ni baada ya kufikia malengo aliyowekewa katika mkataba unaomalizika hivi karibuni ya kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na inafika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Taarifa iliyotolewa leo kupitia mitandao ya kijamii ya Simba haijaweka bayana malengo mapya ambayo kocha huyo amepewa.

Comments are closed.