The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: DKT. MSOLLA MWENYEKITI MPYA YANGA SC

Mwenyekiti mpya wa Dkt. Mshindo Msolla.

Klabu ya Yanga imemchagua Dkt. Mshindo Msolla kuwa mwenyekiti wake huku Fredrick Mwakalebela akishinda katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay Dar es salaam, Dkt. Msola amepata kura 1,276 akimshinda mpinzani wake Dkt. Jonas Tiboroha aliyepata kura 60.

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Mwakalebela amepata kuara 1,206 akiwashinda Janneth Mbene aliyepata kura 61, Titus Osoro aliyepata kura 17, Yono Kevela aliyepata kura 31 na Chota Chota aliyepata kura 12.

Matokeo kamili yakiwemo ya nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji yatakujia hivi punde.

Uchaguzi Mkuu Yanga
Kura za Mwenyekiti
Dr Mbette Mshindo Msola 1276
Dr Jonas Tiboroha kura 60

Kura za Makamu Mwenyekiti
Salum Magege Chota 12
Titus Osolo 17
Yono Kevela 31
Janet Mbene 67
Fredrick Mwakalebela 1206

.

Comments are closed.