BREAKING NEWS: FATMA KARUME ASHINDA URAIS WA TLS

WAKILI wa kujitegemea, Fatma Karume amechaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Lawyers Society – TLS), akichukua mikoba ya aliyekuwa Rais wa Chama hicho, Tundu Lissu baada ya muda wake kumalizika.


Katika uchaguzi huo, Dkt. Rugemeleza Nshala amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa chama hicho.

Aidha, Ndugu Omar Shaaban amechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar Lawyers Society.


Kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho, Uongozi wa TLS hudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, na baada ya hapo viongozi wengine huchaguliwa.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Arusha, Kamati ya Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, (TLS) iliyoundwa kujadili uamuzi wa Mwanasheria wa Mkuu wa Serikali (AG)wa kuzifanyia mabadiliko kanuni za uchaguzi wa chama hicho imesema, AG hakuwa na mamlaka ya kufanya mabadiliko yoyote.

Makamu wa Rais wa TLS ambaye amemaliza muda wake, Godwin Ngwilimi, ametoa hoja hiyo na kumtaka mjumbe wa Baraza la uongozi, Jeremiah Mtobesya kusoma mapendekezo hayo ambayo yalisema Mwanasheria Mkuu wa serikali hakuwa na Mamlaka ya kufanya mabadiliko bali kuyachapisha kwenye gazeti la serikali.

Pia walipendekeza kufuata njia za kiutawala kuonana na Mwanasheria Mkuu au kwenda mahakamani kutafuta tafsiri ya mamlaka yake kwa TLS.

Aidha, Fatma Karume amesema maboresho yaliyofanywa hayana msingi wa kisheria kwa kuwa kanuni za uchaguzi wa TLS zinaanza kufanya kazi mara tu baada ya kupitishwa na mkutano mkuu. Hata hivyo wajumbe hao walikubaliana na baraza la uongozi kutengeneza kanuni ambazo zitatamka kuwa si lazima zitangazwe kwenye gazeti la serikali ili ziwe halali.

MAZITO ! FATMA KARUME AIBUKA, SIOGOPI VITA ,NAJIAMINI

“Mshaurini Rais, Kikwete Alikuwa Mbunifu” – Chacha Rioba

Loading...

Toa comment