The House of Favourite Newspapers

BREAKING: MNANGAGWA ASHINDA URAIS ZIMBABWE

Rais mteule wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa.

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Zimbabwe (ZEC) usiku wa kuamkia leo imetangaza matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zimbabwe, baada ya uchaguzi mkuu kufanikiwa kufanyika salama Julai 30,  2018.

 

Emmerson Mnangagwa wa Zanu-PF ameshinda Urais wa Zimbabwe katika uchaguzi wa kwanza wa Urais, baada ya Robert Mugabe kuondoka madarakani, Mnangagwa ameshinda kwa kupata zaidi ya aslimia 50 ya kura zote dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa kutoka MDC.

 

ZEC wametangaza kuwa Emmerson anashinda kiti hicho kwa kupata ushindi wa asilimia 50.8 ya kura zote halali zilizopigwa wakati mpinzani wake wa karibu kutoka MDC Nelson Chamisa akipata asilimia 44.3 ya kura zote.

Comments are closed.