The House of Favourite Newspapers

Breaking: Sarri Rasmi Atua Juventus, Aondoka Chelsea

Hatimaye leo  Juni 16, 2019 Juventus, wamemtangaza Sarri kuwa kocha wao mpya, akisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuinoa timu hiyo akichukua mikoba ya Max Allegri, aliyeachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita. Chelsea pia imethibitisha kocha wake Maurizio Sarri ameondoka katika timu hiyo akienda zake kuinoa Juventus.

Sarri amedumu kwenye kikosi cha Chelsea kwa miezi 11 huko Stamford Bridge, akiwaongoza kubeba ubingwa wa Europa Ligi na kuwarudisha kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita.

Comments are closed.