The House of Favourite Newspapers

Cardi B Aja Na Product Mpya Sokoni,Boys & Girls Kazi Kwenu!! (PICHA)

Kwa mara ya kwanza rapa Cardi B amezindua mavazi yake ambayo wameshirikiana na kampuni kubwa ya mavazi duniani, ‘Fashion Nova’.

 

Uzinduzi huo umefanyika jana usiku Novemba 14  huko Los Angeles ambapo kulikuwa na shoo za wasanii kama City Girls, Saweetie na wengine.

Akizungumza na Jarida la Vogue, Cardi amesema, “Hivi ni vitu ambavyo najiona mwenyewe nimevaa kwenye miaka ya 60 na 70,  nilikuwa nafikiri ni kitu gani ningevaa wakati wote, kama tunazo jaketi  nyingi, tunazo rangi za giza nyingi, miakanda, rangi za bluu.  Hakuna kinachong’aa…”

 

Wiki iliyopita Cardi B alitangazwa rasmi kuingia mkataba na kampuni kubwa ya mavazi  na viatu ya Reebok.

 

  • ISIKUPITE:”BWANA WA HAMISSA MOBETO NI TAPELI

 

Comments are closed.