The House of Favourite Newspapers

CCM Yafanya Marekebisho Juu ya Ratiba ya Mchakato Wa Ndani wa Uteuzi wa Wagombe Ubunge na Udiwani

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi. (Picha na Maktaba)

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya marekebisho juu ya ratiba ya mchakato wa ndani wa uteuzi wa wagombea wa nafasi ya ubunge, ujumbe wa Baraza la wawakilishi na udiwani, kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.