The House of Favourite Newspapers

Championi, Spoti Xtra Yamwaga Zawadi ya Vitabu vya Shigongo

0

DROO ya kwanza ya promosheni ya Shinda Zawadi ya Kitabu cha Shigongo, imefanyika leo Novemba 10, 2021 ambapo jumla ya washindi watano wamepatikana, huku Dar es Salaam ikiongoza kutoa washindi wengi.

 

Kwenye droo iliyochezeshwa na kuoneshwa moja kwa moja kupitia Global TV, ilitoa washindi ambao ni Khalid Katto Ismail, Richard Mbano, Philemon Kevin na Khadi Mussa wote wakazi wa Dar es Salaam, huku mshindi mwingine akiwa Philip Simon Mlimangano kutoka Tabora.

 

Magazeti ya Spoti Xtra na Championi, yamekuja na promosheni kabambe kwa wasomaji wake ambapo kupitia magazeti hayo msomaji ataweza kujipatia bure moja ya vitabu vya mwandishi mahiri, Eric Shigongo.

 

Kwa kununua Gazeti la Spoti Xtra linalouzwa Sh 500 kila siku za Jumanne, Alhamisi na Jumapili, sambamba na Championi linalopatikana Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi kwa Sh 800, unapata fursa ya kujishindia moja ya vitabu vya Eric Shigongo.

 

Miongoni mwa vitabu hivyo ni Rais Anampenda Mke Wangu, Kifo ni Haki Yangu, Machozi na Damu na vingine vya ujasiriamali.

HUSSEIN MSOLEKA

Leave A Reply