The House of Favourite Newspapers

Championi Yamtunuku Nyota wa GOLF, Amwaga Machozi – Video

Nyota wa golf, Angel Eaton, akiwa na tuzo aliyopewa na Championi leo.  Pamoja naye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo (wa pili kushoto), Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kulia) na Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Global Publishers, Saleh Ally.

MTANZANIA ambaye ni nyota wa mchezo wa golf Afrika Mashariki, Angel Eaton, amejikuta akimwaga machozi baada ya kukabidhiwa tuzo ya heshima kutoka Kampuni ya Global Group kupitia gazeti namba moja la michezo la  Championi kwa kutambua juhudi ambazo anazifanya.

 

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho,  akimkabidhi Angel Eaton, Tuzo ya Heshima kutoka magazeti ya Championi.

Angel amekabidhiwa tuzo hiyo na Meneja Mkuu wa Global  Publishers, Abdallah Mrisho, wakati wa hafla fupi aliyoandaliwa na kampuni hiyo iliyopo Sinza-Mori jijini Dar kwa ajili ya kutambua mchango wake kwa taifa katika tasnia ya mchezo wa golf nchini.

 

…Akimwaga machozi wakati akizungumza baada ya kupewa tuzo hiyo.

Akiwa ofisini hapo nyota huyo ambaye ameshinda makombe 34 ya mchezo huo katika nchi mbalimbali za Afrika, alitembelea vitengo mbalimbali vikiwemo studio za Global TV, +255 Global Radio  na ofisi za magazeti ya Championi na Magazeti Pendwa.

…Akiishukuru kampuni ya  Global kwa tuzo hiyo kwa kutambua anachokifanya.

Jina la Angel Eaton siyo geni masikioni mwa wadau wa michezo ndani na nje ya Afrika Mashariki na Kati na umaarufu wake umetokana na kazi nzuri anazofanya uwanjani, katika safari ya kuiwakilisha vema klabu yake ya Lugalo na Tanzania.

…Akionyesha vitendea-kazi vyake wakati akizungumza na wafanyakazi wa Global.

Mwanadada huyo alizaliwa mwaka 1990 katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja wa kike anayefahamika kwa jina la Delight.

Mhariri Mwandamizi, Walusanga Ndaki (kushoto)  akimuuliza swali Angel.

Angel anamiliki makombe mengi aliyotwaa kupitia mchezo huo yakiwemo ubingwa wa 2006 baada ya kutwaa Tanzania Ladies Open, mwaka 2007, Mwalim Julius Nyerere (Overall Winner), CDF Cup, Uganda Ladies Open na Dar Gymkhana.

…Akiuelezea mchezo wa golf kwa wafanyakazi wa Global.

Mwaka 2008 alishinda mataji ya Lady Cameroon, Uganda Ladies Open, Tanzania Ladies Open, Leisure Ladies Open na Toyota Golf Cup. Pia makombe mengine anayoshirikia ni Zambia Ladies Open, Uganda Ladies Open aliyoshinda mwaka 2010.

…Akionyesha vifaa vya michezo ya golf.

Mataji mengine ni Mombasa Ladies Open, Morogoro Ladies Open, Tanzania Ladies Open aliyoshinda mwaka 2011 na mwaka huu ameibuka tena kidedea kupitia mashindano yaliyomalizika Machi 14, nchini Malawi.

 

…Akionyesha moja ya vifaa vya michezo.

Akizungumza wakati wa kutoa tuzo hiyo maalumu, Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo,  amesema tuzo hii ni mwanzo wa kutambua mchango wa watu wenye mchango chanya kwenye jamii katika nyanja mbalimbali ili kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kuwakumbuka watu waliolifanyia na wanaolifanyia mambo mema taifa hili.

Shigongo akizungumza jambo.

Kwa upande wake Angel mwenye tuzo 34 za mchezo huo, mbali na kuishukuru kampuni ya Global Group ameomba utaratibu wa kuwatambua watu wenye kuiletea tija na sifa jamii, kugusa tasnia nyingine ili kuwainua wahusika na taifa kwa jumla.

 

Historia fupi ya Angel Eaton

JINA la Angel Eaton, si geni masikioni mwa wadau mbalimbali wa michezo ndani na nje ya Bara la Afrika Mashariki na Kati, umaarufu wake umetokana na kazi nzuri anazofanya uwanjani, katika safari ya kuiwakilisha vema klabu yake ya Lugalo na Tanzania kwa ujumla.

Akionyesha tuzo yake.

Mwanadada huyu alizaliwa mwaka 1990 katika hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam, anatokea katika kabila la Wamakonde lakini pia, ni mama wa mtoto mmoja wa kike anayefahamika kwa jina la Delight.

zxMwaka 2006, ulikuwa mwanzo wake wa kujifunza mchezo wa gofu akiwa katika klabu ya Gymkhana jijini hapa kabla ya 2014 kuhamishia virago vyake katika klabu ya Lugalo, anayoitumikia hadi sasa.

Angekl akimwaga machozi.

Mashindano aliyochukua ubingwa

2006– Aliwahi kushinda  kupitia mashindano ya ‘Tanzania Ladies open’ (Overall Winner), na mengine mengi ya ndani na nje ya nchi.

Picha ya ukumbusho na Shigongo. 

 

2007– Alishinda mashindano ya Mwalimu Julies Nyerere (Overall Winner)

-CDF Cup

-Uganda Ladies Open

-Dar   Gymkhana Trophy nakadhalika

Akiwa na wafanyakazi wa Global.

2008– Lady Cameroon Cup

-Uganda Ladies Open

-Tanzania Ladies Open

-Leisure Ladies Open

-Toyota Golf Cup, nakadhalika

2010– Zambia ladies Open

-Uganda Ladies Open, n kadhalika

czx2011- Mombasa Ladies Open

-Kenya Ladies Open

-Uganda Ladies Open

-Morogoro Ladies Open

-Tanzania Ladies Open, nakadhalika

2012– Uganda Ladies Open

-Tanzania Ladies Open, nakadhalika.

2016– Uganda Ladies Open

-Nairobi Ladies Open, nakadhalika

2018– aliibuka kidedea nchini Nigeria

2019– aliibuka bingwa wa mashindano ya wanawake nchini Malawi.

 

EXCLUSIVE: “Sijawahi Kufanyiwa Kitu Kama Hiki” – ANGEL EATON

Comments are closed.