The House of Favourite Newspapers

Chid Benz Akamatwa Tena na Madawa ya Kulevya

0

RAPA Rashid Makwiro maarufu kama Chid Benz na wenzake saba, wamekamatwa na Jeshi la Polisi tangu Jumamosi baada ya kukutwa na dawa za kulevya maeneo ya Kariakoo jijini Dar, ikiwa ni siku chache baada ya kuhusishwa kurudia matumizi ya madawa hayo.

Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba msanii huyo na wenzake wanaendelea kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Msimbazi kwa mahojiano na upelelezi zaidi.

Tukio hilo limetokea siku chache baada ya Chid Benz kurejea uraiani, akitokea sobber house alikopelekwa baada ya kutopea kwenye matumizi ya madawa hayo, kiasi cha afya yake kuyumba sana.

Soma habari Kamili Kesho katika Gazeti la Risasi Mchanganyiko.

Leave A Reply