The House of Favourite Newspapers

ads

Chongolo Ataka Kiwanda cha Kilombero Kitoe Elimu kwa Wakulima wa Miwa

0

 

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatuma Mwassa kukutana na uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kwa lengo la kuandaa mafunzo maalum kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika na Masoko (AMCOS) vyote vilivyopo Wilaya ya Kilombero ili kuweza kuwapa mafunzo ya kujua kiwango cha sukari kilichopo katika miwa ambayo inatumika kuzalisha sukari.

 

“Kila Amcos itoe muwakilishi mmoja mmoja ili wakapate elimu ya kufahamu vipimo vya kiwango cha sukari kwenye miwa yao wakati wa upimaji, jambo hili litaondoa malalamiko kwa wakulima kuwa wanapunjwa kiasi cha fedha wanazolipwa kutoka kiwandani. Fanyeni hivyo mapema,” amesema Chongolo.

 

 

Awali, Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Abubakari Asenga alitoa malalamiko hayo mbele ya Chongolo wakati akizungumza na wafuasi wa CCM Msolwa A na B, Januari 30, 2023 wakati wa muendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya CCM.

Leave A Reply