The House of Favourite Newspapers

CHUO CHA PCTL KUTOA KOZI MAALUM KUWAANDAA WAHITIMU KUPATA AJIRA

Tatizo linaliowasumbua wasomi wengi wanaohitimu kwenye vyuo mbalimbali nchini, ni kukosa sifa za kuajiriwa licha ya kuwa na elimu ya kutosha, hali inayosababisha tatizo la ukosefu wa ajira kuzidi kuwa kubwa miongoni mwa vijana.

 

Kutokana na changamoto hiyo, Chuo cha PCTL Training Insitute kimeanza kutoa kozi maalum za kuwapiga msasa wahitimu kutoka vyuo vikuu na vyuo vingine, kupata ujuzi wa ziada wa masuala ya teknolojia ili iwe rahisi kuajiriwa ndani na nje ya nchi.

Chuo hicho kilichopo Ghorofa ya 10 katika Jengo la Sabodo Parking, Mtaa wa India, Posta jijini Dar es Salaam, kinatoa kozi mbalimbali zikiwemo Computer Essentials, Information Technology, IT Security, Digital Marketing Computing, Tally na kadhalika ambazo ni muhimu katika soko la ajira.

 

 

PCTL pia wanatoa kozi za awali kwa watu wa aina zote wanaopenda masuala ya teknolojia kuanzia ngazi za chini kabisa, huku mwanafunzi pia akifundishwa Lugha ya Kiingereza na kuandaliwa kuja kuwa mbobezi katika masuala ya Tehama, kwa ada nafuu kabisa.

 

Kwa maelezo zaidi, unaweza kuwasiliana nao kwa namba za simu: 0655 489 473 au 0755 489 473, kwa barua pepe kupitia [email protected] au unaweza kutembelea tovuti yao kwa kubofya www.pctl.co.tz.

 

Comments are closed.