#GlobalCelerbrityUpdates: Ciara Kwenye Pozi Nane Tofauti Kipindi Hiki Cha Ujauzito – (Pichaz)

 

Staa wa muziki kutoka Marekani Ciara ambaye kwa sasa ni mjamzito amefanya interview na jarida la Harper Bazaar na kuzisogeza kwetu picha nane akiwa kwenye pozi tofauti kutoka kwenye interview hiyo.

Ndani ya interview hiyo Ciara ameongelea maisha yake ya ndoa na mwanamichezo Russell Wilson, muziki wake, pamoja na maandalizi anayofanya kujianda kumleta duniani mtoto wake wa pili.

Feel free kuzipitia picha zote moja baada ya nyingine hapa chini.

Ciara amelezea jinsi ambavyo mwanae ‘baby Future’ anauchukulia ujauzito wake:

Ana shauku kubwa ya kumuona mtoto. Mara nyingi ananishika tumbo na kusema ‘nataka kumuona mtoto’. Mara atanifuata na kusema ‘Hello toto, unaendeleaje? I love you toto. Okay, nitaongea na wewe badaae toto. Bye Bye’. Wakati mwingine atakuja na kunibusu tumboni na kuondoka…

 

 

 

Anachukuliaje maisha ya kuwa mama na amejiandaa vipi kumkaribisha duniani mtoto wake wa pili?:

Nipo very excited na maisha yangu ya sasa. Sijui nikuambiaje! Kumuona mwanangu anakimbia kimbia kila kona ya nyumba inanipa faraja kubwa sana na very soon watakuwa wawili wakikimbizana mle ndani! Maisha yetu yatakuwa kukimbizana mwanzo mwisho.” 

Unaweza kuipitia interview nzima ya Ciara na Harper Bazaar kwa kubonyeza hii link ya blue.

 

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine zikufikie kwa wakati.
Toa comment