The House of Favourite Newspapers

Dada Auawa Kwa Kupigwa Risasi Katika Mzozo Wa Zawadi Ya Krismasi Florida

0

Ndugu wawili wamekamatwa baada ya dada yao kupigwa risasi na kuuawa wakati wa mabishano kuhusu zawadi za Krismasi.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 alipigwa risasi kifuani na kakake huku akiwa na mtoto wake wa kiume wa miezi 10 kwenye gari la kubebea mizigo, polisi mjini Florida ilisema.

Mvulana huyo baadaye alipigwa risasi na kaka yake mkubwa ambaye alichukua bunduki yake mwenyewe, Ofisi ya Sheriff wa Kaunti ya Pinellas ilisema

Iliongeza kuwa kisa hicho cha ufyatulianaji risasi kilifuatia mabishano juu ya nani alikuwa akipokea zawadi zaidi.

Sheriff Bob Gualtieri aliwaambia waandishi wa habari kwamba kijana mkubwa, mwenye umri wa miaka 15, alikimbia kutoka eneo la tukio na kutupa bunduki yake.

Ndugu mdogo, mwenye umri wa miaka 14, alipelekwa hospitalini na yuko katika hali nzuri na atawekwa chini ya ulinzi atakapotolewa hospitaliu, polisi walisema.

Waendesha mashtaka wa eneo hilo watatathmini kesii hiyo ili kuamua iwapo watamfungulia mashtaka kama mtu mzima kwa mauaji ya dada yake, Mamlaka ya pilisi ya Gualtieri iliongeza.

Mwanamke huyo alipelekwa hospitalini, ambapo alitangazwa kuwa amekufa, Sheriff Gualtieri alisema.

Kaka yake mwenye umri wa miaka 15 alikamatwa na kushtakiwa kwa jaribio la mauaji na kuficha ushahidi.

MUNGU WANGU! JIRANI NDIYE ALIYEWAUA WATOTO 7 KWA SUMU BAADA ya KUIBIWA JOGOO WAKE KAGERA, RPC AELEZA

Leave A Reply