The House of Favourite Newspapers

DALILI ZA MPENZI ASIYEKUPENDA

Image result for couples arguing

KATIKA uhusiano wa kimapenzi, kumpenda mtu ni jambo la kwanza na uliyempenda kukupenda wewe ni jambo la pili na jambo la tatu ni kupendana na kuridhiana. 

 

Nitumie fursa hii kukutia moyo wewe ambaye una maumivu ya mapenzi kwa kumpoteza mtu uliyempenda sana na kukosa raha tena ya mapenzi na maisha. Katika uhusiano wa kimapenzi, kumsahau mtu uliyempenda, aliyekuacha ukiwa bado unampenda ni vigumu mno ila inawezekana kama utakubali ulimpenda, akakupenda na sasa si wako tena.

Baada ya kukutana na hali hiyo, tumia nafasi hiyo kujiamini, kujithamini, kujipenda binafsi na kuwa na msimamo katika mapenzi na maisha yako kwa jumla. Jenga furaha mpya kwani si mwisho ila ni mwanzo wa maisha mapya, hali hiyo itakupa tumaini jipya na nafasi ya kumuona akupendae kwa dhati katika mapenzi yako na kukupa thamani ya vile ulivyo katika mapenzi na maisha yake.

 

Unajua unaweza kuwa na uhusiano na mtu unayempenda sana ila yeye hakupendi kama vile umpendavyo, lakini anashindwa kukwambia kuwa ‘SIKUPENDI’.

Hapa ninakujuza kuwa una wakati mzuri sana wa kumtambua mtu ambaye hakupendi na pia kumtambua anayekupenda. Vilevile kukubaliana na hali halisi. Watu wengi hawapendi kutambua kwamba mtu anayempenda yeye hampendi kwa sababu ni maumivu makubwa sana moyoni.

Unapokuwa kwenye uhusiano na mtu huyo naye inamuwia vigumu kukwambia ‘SIKUPENDI’, hufanya hivi katika kuzihurumia hisia zako juu yake. Katika makala hii zifuatazo ni dalili za mtu ambaye hakupendi kwa dahati;

MOJA

Anapokuwa na wewe inamuwia vigumu sana kukwambia neno ‘NAKUPENDA’ mara kwa mara, utajikuta wewe ndiye unakuwa mtumwa kwake kwa kumwambia nakupenda kila mara. Majibu yake baada ya neno hilo, mara nyingi atakwambia asante kwa kunipenda basi na akikuhurumia sana atakwambia nakupenda pia ili kukuridhisha wewe na moyo wako.

MBILI

Utajikuta una mawazo sana juu yake na kujiuliza ‘hivi kweli mtu huyu ananipenda?’ Utajaribu kumuuliza, ‘je, unanipenda?’ Jibu lake kwanza atalifikiria sana. Sababu ya kufanya hivyo ni kwa vile anatambua kwamba hakupendi, sasa kukwambia ukweli wa swali lako anahisi utaumia. Kwa hiyo baada ya swali hilo anaweza kukuuliza swali na wewe, ‘kwani unaonaje?’ Kwa vile unampenda sana utamjibu, ‘naona kuwa unanipenda’ naye atakwambia, ‘basi ndiyo hivyo’.

Mara nyingine baada ya wewe kumuuliza swali kuwa je, anakupenda kweli, atakujibu, ‘ukweli unaujua ila kwa nini unapenda kuniuliza swali hilo kila mara?’ Kama umeshaingiza dosari juu ya upendo wake utajikuta unamuuliza, ‘ukweli upi?’ Naye atakujibu, ‘kuwa nakupenda’. Hapo utajikuta umepata furaha kugundua kuwa anakupenda, kumbe mwenzio amekuhurumia tu.Image result for couples arguing

TATU

Huwa hajali mambo yako unayomwambia, ukimweleza muda huu baadaye anajifanya kusahau ili tu akupotezee mwelekeo.

NNE

Unapopanga kukutana naye huwa ni mtu asiyeishiwa na sababu za kushindwa kufika. Huwa na aibu ya kukutambulisha kwa watu. Unaweza kufika naye mahali akakwambia kuwa, ‘kuna watu wanafahamiana na mama au baba mahali hapa kwa hiyo tusiongozane karibu’. Hapo anaweza yeye akatangulia mbele au kukuacha wewe utangulie.

TANO

Hufanya tabasamu la kuigiza au kicheko cha kejeli ili wewe uridhike kwamba anafurahishwa na uwepo wako kwake. Wakati mwingine inampasa mtu kujitambua na kumpa uhuru huyo umpendaye aweze kuamua mwenyewe labda kuendelea na wewe au kumfuata anayempenda yeye. Cha muhimu ni kuwa using’ang’anie uhusiano ambao unakuumiza moyo kwani unaweza kupasua moyo wako kwa mawazo.

Kwa maoni, nicheki kwenye namba hapo juu au tembelea ukurasa wetu wa Gazeti la Ijumaa Wikienda kwenye Facebook.

Masaa 3 Lema Kuhojiwa POLISI Kuhusu MO Atoka na Kutema cheche

Comments are closed.