Daniel Chapo wa chama Cha Frelimo Ashinda Urais Msumbiji

Tume ya uchaguzi nchini msumbiji CNE, imemtangaza Daniel Chapo kutoka chama Cha Frelimo, kuwa Rais mteule wa taifa hilo baada ya kushinda Kwa asilimia 70 za kura dhidi ya mpinzani wake wa karibu Venancio Mondlane aliyepata asilimia 20 ya kura katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 9 mwaka huu .
Daniel Chapo anachukua nafasi ya Filipe Nyusi kutoka chama Cha Frelimo, anayeondoka madarakani baada ya miaka 10, akishika nafasi hiyo tangu mwaka 2014 baada ya kuhudumu kama Waziri.
Daniel Chapo alihudumu kama Gavana wa inhambane kuanzia mwaka 2016 mpaka 2024, akiwa na taaluma ya Sheria pia.