The House of Favourite Newspapers

DJ KHALED, MCHUMBA’KE WAANGUSHA BETHIDEI YA KUFA MTU!

DJ Khaled  na mchumba wake,  Nicole Tuck, wiki iliyopita waliadhimisha siku zao za kuzaliwa kwa kishindo kikubwa kilichojumuisha saa za mkononi za bei mbaya.  Wawili hao huadhimisha pamoja kumbukumbu hizo ambapo Khaled alifikisha miaka 43  Novemba 26 na Nicole alifikisha miaka 43 siku ya Ijumaa iliyopita ambapo sherehe ya kufa mtu ilifanyika ukumbi wa Perez Art Museum huko Miami ambapo sherehe iliyokutanisha watu 60 ilifanyika, wakiwemo marafiki na wanafamilia.

Kivutio kikubwa hapo kilikuwa ni saa zenye thamani kubwa ambapo ile ya Khaled ilikuwa ni  Roger Dubuis Excalibur iliyoharimu Dola elfu 106 (Sh. milioni 243) na ya Nicole aina ya  Roger Dubuis Velvet Caviar, iligharimu Dola elfu 53 (Sh. milioni 122).  Saa zote hizo zimenakishiwa kwa madini ya almasi.

Khaled hivi sasa ana saa kibao za aina hiyo nyumbani kwake na mwaka jana Nicole alitengenezewa saa maalum yenye vipande 600 vya almasi ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya mtoto wao, Asahd, aliyekuwa anasherehekea mwaka mmoja.

Sherehe hizo zilihamia klabu ya LIV ambako burudani kubwa ya muziki iliangushwa na mastaa mbalimbali wakiwemo  Swizz BeatzFat JoeBusta RhymesYoung Jeezy na Fabolous.

Credit: Tmz

Comments are closed.