The House of Favourite Newspapers

Dkt. Nchimbi Aifariji Familia ya Aliyekuwa Katibu wa CCM Rombo

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na familia ya aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Bi. Mary Sulle, alipofika kuwapatia pole na kuwafariji. Bi Sulle aliyefariki usiku wa kuamkia tarehe 18 Machi 2025, anatarajiwa kuzikwa Ijumaa Machi 21, 2025, nyumbani kwao Karatu.