The House of Favourite Newspapers

Dullah Mbabe Ashinda Ubingwa wa Dunia kwa TKO China – Video

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’, jana mchana alifanikiwa kumchapa kwa TKO ya raundi ya tatu, Zulipiker Maimaitiali,  raia wa China na kushinda Bingwa wa Dunia wa bara la Asia ‘WBOAP’ uzito wa kati.

 

Katika pambano hilo ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa TSSG, Qingdao, China,  ambalo lilikuwa la raundi kumi, Mbabe amefanikiwa kushinda katika raundi ya tatu kwa TKO.

 

Mbabe ameshinda pambano hilo ambalo limechezeshwa na mwamuzi wa kati, Sawaeng Thaweekoon, huku majaji wakiwa Edward Ligas, Surat Soikraching na Mekin Sumon.

 

Bondia huyo ameliambia Championi Jumamosi: “Nimefanikiwa kushinda ubingwa wa dunia huku China, namshukuru Mungu.  Naomba Watanzania wafike kwa wingi uwanja wa ndege siku ya Jumatatu kuchukua ubingwa ambao wamenituma,”

Comments are closed.