The House of Favourite Newspapers

Emmanuel Mbasha Amkana ‘Mchumba’ke’

1

 

BAADA ya kudaiwa kumvisha pete ya uchumba mshiriki wa Miss Tanzania 2008, Jacqueline Chuwa ‘Jack’, Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha amemkana akidai hamfahamu mlimbwende huyo.

 

Akipiga stori na Za Motomoto News, Mbasha alisema hamfahamu msichana huyo na kwamba hana mchumba wala rafiki wa kike kwa sasa, akisema picha ambayo alipiga akiwa dukani na shela, ilikuwa ni kwa ajili ya kuomba miujiza kutoka kwa Mungu ili apate mke mwema.

 

“Sina mchumba wala mpenzi na picha niliyoweka kwenye ukurasa wangu wa Instagram niliamua kupiga nikiwa nimeshika tu shela ili Mungu afanye jambo kwangu, nikipata mchumba nitawaambia mashabiki wangu wala wasijali kwa hilo, huyo Jack simfahamu,” alisema Mbasha.

1 Comment
  1. […] wa nyimbo za Injili Tanzania, Flora Mbasha amevunja ukimya na kutoa onyo kwa baadhi ya watu wanaomchafua kupitia […]

Leave A Reply