×

Eng. Hersi Atamba na Usajili Mpya

MJUMBE wa Kamati ya Usajili ya Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said, ametamba kuwa kwa usajili mpya na wa kisasa wanaoendelea kuufanya unampa matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA msimu wa 2020/21.

 

Kauli ya bosi huyo wa GSM imekuja baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji wawili wa kimataifa wanaokipiga AS Vita ya DR Congo, winga Tuisila Kisinda na kiungo mkabaji, Mukoko Tonombe.

 

Wachezaji wengine wapya waliosajiliwa na Yanga ni Yacoub Sogne, Yassin Mustapha, Farid Mussa, Zawadi Mauya, Kibwana Shomari, Bakari Mwamnyeto, Waziri Junior na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Hersi alisema kuwa usajili wao wanaoendelea kuufanya umezingatia ubora wa mchezaji katika kuhakikisha wanatengeneza timu ya makombe.Hersi alisema, hadi sasa hakuna sehemu waliyokosea katika usajili wao baada ya kuwapata wachezaji bora waliokuwepo kwenye kiwango kikubwa kutoka AS Vita ambao ni Tonombe na Tuisila.

 

Aliongeza kuwa bado wanaendelea kukiimarisha kikosi chao na hivi sasa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa washambuliaji wawili wote kutoka nchini Angola.

 

“Kama nilivyoahidi kabla ya msimu uliopita kumalizika lazima tuuchukue ubingwa wa ligi msimu ujao na ili tufanikishe hilo tumepanga kufanya usajili wa wachezaji bora watakaotupa ubingwa.

 

“Hivyo, basi kama wadhamini tumeona tuchukue jukumu hili la kufanikisha usajili katika msimu ujao kwa kusajili wachezaji bora waliokuwepo kwenye mipango yetu.

 

“Hiyo ndiyo sababu ya kufanikisha usajili wa wachezaji wazuri walio kwenye kiwango bora kutoka AS Vita ambao ni Tonombe na Tuisila, kiukweli haikuwa rahisi kufanikisha usajili huo kutokana na wachezaji hao kuwa na mikataba na klabu yao,” alisema Hersi.

 

Kutokana na kauli hiyo, ni wazi Tuisila na Tonombe wana majukumu makubwa ya kufanikisha Yanga inatwaa makombe hay

Leave a Comment