ENZI ZA UTOTONI, UNAAMBIWA KAJALA ALIKUWA HAOGI

Ukiona mastaa Bongo sasa hivi wanajipenda na kupendeza ni vigumu kujua huko nyuma walikuwa wengine hata wanarudi nguo siku nzima.

 

Sikia hii ya mwigizaji mahiri wa Bongo Muvi, Kajala Masanja ambaye ukimuona sasa hivi ni mwanamke anayejipenda na kunukia kila wakati, lakini huko nyuma unaambiwa ilikuwa mbinde kuoga.

 

Akizungumza na Imefunuka ya Ijumaa Wikienda, Kajala alisema kuwa alipokuwa kidato cha kwanza ambapo alianzia shule moja mkoani Songea, kulikuwa na baridi kali kiasi kwamba alikuwa akiamshwa asubuhi kwenda kuoga, akifika bafuni, anakaa kama nusu saa halafu anamwaga maji chini kisha ananawa uso na kutoka.

 

“Mimi na baridi ilikuwa ni vitu viwili tofauti kabisa kwa sababu ilikuwa tukiamshwa asubuhi kwenda kuoga, nacheza mchezo tu, nakaa kwa muda kisha namwaga maji chini. Nilikuwa naweza kupiga hivyo hata wiki nzima labda siku tupate moto tuchemshe maji ndiyo nilikuwa ninaoga,” alisema Kajala.


Loading...

Toa comment