visa

Esha, Mapenzi ya Ebitoke, Mlela siyo kiki

MWANAMAMA anayefanya vizuri kunako Bongo Muvi, Esha Buheti amesema mapenzi ya msanii mwenzake Yusuph Mlela na mchekeshaji, Anastazia Exavery ’Ebitoke’ ni kweli na siyo kiki kama ambavyo watu wanadhani. Akibonga na Za Motomoto ya Risasi, Esha alisema amekuwa karibu kwa kipindi kirefu na Mlela hivyo anamjua vizuri na uhusiano wake na Ebitoke siyo kiki kama ambavyo watu wengi wanafikiria.

“Unajua mimi namfahamu Mlela siku nyingi ni kama kaka kwangu, hivyo hata mimi mwanzoni nilikuwa najua siyo kweli wanatutania lakini mwisho wa siku nikaja kugundua kwamba wapo serious na mapenzi yao na wala siyo kiki,” alisema Esha.
Toa comment